Home | Terms & Conditions | Help

May 4, 2024, 8:07 pm

NEWS: VIWANDA 57 NCHINI VINATUMIA GESI ASILIA

DODOMA: Meneja wa biashara ya Gesi Asilia kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Emmanuel Gilbert ameeleza kuwa viwanda 57 nchini kutika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara,Lindi na Pwani vinatumia Gesi Asilia ambapo awali vilikuwa vinatumia mafuta mazito (Industrial Dizeli).

Akizungumza jijini hapa katika Maonesho ya Wiki ya Nishati kwenye viwanja vya Bunge

alisema kuwa wateja wao wamewaweka katika makundi tofauti ambapo kundi la kwanza ni la kuzalisha umeme ambapo mteja wao mkubwa ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),na kwamba kiasi wanachopeleka TANESCO kinawekuzalisha asilimia 60 ya umeme wote unaotumika hapa nchini unaozalishwa kutumia Gesi Asilimia.

Alisema kuwa wanawateja wa viwanda ambao wanatumia Gesi Asilia kwa matumizi ya viwandani kama kuzalisha umeme wao wenyewe wa kuendeshea shughuli za viwanda na kutumia kama niashati ya kuchoma malghafi mbalimbali katika viwanda vyao badala ya kutumia niashati ya mafuta mazito au dizeli.

" Wanatumia Gesi Asilia kwanza ni bei rahisi lakini pia inatunza mazingira kwa kuwa ikichomea inaungua kwa asilimia 100 na haitoi masinzi, hewa ukaa," alisema.

Aliongeza kuwa wateja wengine wamewaweka katika kundi la matumizi ya kupikia majumbani na baadhi ya taasisi ambazo zinatumia Gesi Asilia kama hotelini, vyuoni pamoja na magereza.

"Kwa mfano Mtwara tuna taasisi nne ambazo zinatumia Gesi Asilia gereza kuu la Lilungu, tumeonganisha nyumba zote za watumishi wa gereza, majiko ya jumuiya ya wafungwa yamehama katika kutumia kuni kwa ajili ya kupikia kwa sasa wanatumia Gesi Asilia pia tumeonganisha sekondari ya Ufundi Mtwara nayo inamtumia gesi hii, chuo cha walimu Ufundi na kwa walimu wa kawaida," alieleza.

Alisema kuwa eneo la nne wanapeleka kwenye vituo ambavyo vinaweza kutoa Gesi kwenye magari huku akifafanua kwamba gesi hiyo inaweza kutumika kuendeshea magari yanayo tumia mafuta ya dizeli au petroli kwa kuwekewa mifumo maalumu zikabalishwa kutoka kwenye matumizi ya mafuta ikatimia gesi hiyo.

Alisema kuwa TPDC wana mradi wa ujenzi wa vituo vya kujazia Gesi Asilia kwenye magari na kwa sasa tayari wameshapa mkandarasi wa kujenga kituo kimoja kikubwa jijini Dar es Salaam .

Alifafanua kuwa kituo hicho kitakapokamilika kitajuwa na uwezo wa kujaza Gesi Asilia kujaza magari 16 kwa wakati mmoja ambazo zitakuwa zimewekewa mfumo wa gesi hiyo.

Aidha alisema kuwa wanakaribisha sekta binafisi waende kuwekeza kwenye ujenzi wa vituo vya kujazia Gesi Asilia kwenye magari huku akisema tangu walivyofungua mlango miaka mitatu ya kuwakarisha wawekezaji tayari vituo viwili vimeshajengwa.