Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 12:11 pm

RC MTAKA: WALIMU RUKSA KUFUNDISHA TUITION

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony John Mtaka ametoa rukhsa kwa Walimu mkoani humo kufundisha Wanafunzi muda wao wa ziada ili kupandisha viwango vyao vya taaluma katika Mkoa huo pamoja na kukuza vipato vya walimu hao.

Mtaka ametoa rukhsa hiyo katika kikao cha uzinduzi wa vitabu vya mwongozo wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa bila kuvunja sheria huku akidai kuwa haoni haja ya kuwazuia kuwa na Tuition binafsi Walimu wakati Kada nyingine wakiwemo Madaktari wamekuwa wakiongeza vipato vyao kwa kuwa na maduka ya dawa.

“Walimu wa Njombe unapomaliza muda wangu wa Serikali nenda kwenye ratiba yako binafsi ili tugawane namna ya kuwaondolea Watoto ujinga kwenye vichwa vyao, fundisheni Mimi nimewapa rukhsa, wakiwauliza waambieni RC ametoa rukhsa sio Afisa Elimu”

Mtaka amesema hataki kuona Mwalimu akifa Masikini kwakuwa Madaktari wamekuwa na maduka ya dawa, zahanati na wanatibu zaidi ya Hospitali mbili hivyo haoni haja ya kuwazuia walimu kuwa na Tuition ili kujiongezea vipato vyao.