Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 8:47 am

NEWS: WAZEE KUNYWA POMBE KUSAHAU LISHE

CHEMBA: Wazee waishio maeneo ya Vijijini wamesema unywaji wa pombe uliokirithi hupelekea baadhi ya Wazee kutozingatia lishe nakupendekeza kuwepo kwa semina nyingi ambazo zitatoa elimu ili kupunguza changamoto hiyo.

Pia, wameiomba Serikali kupitia bunge lake kupitisha sheria ya kuwatambua na kuwalinda wazee zaidi ya sera za wazee zilizopo kwa sasa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Baraza la Wazee Chambalo Seleman Lumambo wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani yaliyoandaliwa na shirika lisilo la Kiserikali la DORCAS AID INTERNATIONAL TANZANIA katika Kijijini cha Chambalo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.

Maadhimisho hayo yaliyoambata na ugawaji wa bima za afya kwa wazee 250 pamoja na vifaa vya shule kwa wanafunzi 250 wa shule za Msingi.

Katibu Lumambo amesema wazee kutokupata chakula cha kila siku kunatokana na kushindwa kujishulisha na kazi za kujipatia kipato wakati huo wana watoto wanaishi mjini Dodoma na mikoa mingine huku wakidai kuwasahau wazee wao.

‘’Kuna wazee wenzetu wanaunga mkono ukeketai , ndoa za utotoni ili kujipatia fedha, hata hivyo bado katika Kijiji chetu cha Chambalo kuna kuna watu/ wazee wengi ambao bado wanaamini kwenye Imani za kishirikina , Kwenda kwa waganga wa kiyenyeji pindi wanapougua badala yakwenda hospitali ambayo wakati mwingine husababisha vifo visivyo vya lazima,’’amesema Lumambo.

Akizungumzia suala la bima baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wazee kukosa huduma za afya za uhakika kutokana na kutokuwa na uwezo wakumudu gharama za matibabu Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon Chacha alisema serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha wazee wanapata matibabu , na kuwaandalia dirisha maalumu kwenye vituo vya afya mbalimbali.

Mratibu wa mradi wa Community Safety net Project kutoka shirika la Dorcas Aid International Tanzania Godluck Kivuyo amesema wameamuwa kuwasaidia wazee kwa kuwapatia bima za afya ili kuamsha ali kwa wadau wengine kuwasaidia wazee hasa maeneo ya Vijijini.

Shirika la Dorcas International Tazania Kijiji cha Chambalo limefanikiwa kupata miradi miwili yaani Mradi wa Watoto 150 na mradi wa wazee 160 waliopo katika mazingira magumu,ambao mpaka sasa wamefadhiliwa.

‘’Lengo la mradi huo ni kuwasaidia wazee wanaoishi katika hali duni , kuwapa tumaini wazee waliokata tamaa kwa kuwaunganisha na jamii zao pamoja na huduma mbalimbali ikiwemo huduma za afya,’’amesema.