Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 9:23 am

NEWS: WALIMU DARASA 3 NA 4 WAFANYIWA TAFITI NA TATHIMINI NA ADEM.

DODOMA: Katika kipindi cha mwaka 2020/2021,Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa elimu na usimamizi wa elimu (ADEM) umefanya tafiti mbalimbali zikiwemo za tathimini ya matokeo ya Mafunzo ya KKK kwa Walimu wa Darasa la III na IV yaliyofanyika Tanzania Bara.

Pia Wakala umefanya utekelezaji wa udhibiti ubora wa shule na utoaji wa mrejesho kwa walimu ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji katika shule za Msingi.

Haya yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa elimu (ADEM) Dkt Siston Mgullah wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya wakala huo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Alieleza Majukumu mengine ni kufanya tafiti katika maeneo ya uongozi na usimamizi wa elimu ili kubaini na kutafuta ufumbuzi wake, kuandaa na kusambaza makala na machapisho ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu.

“Wakala inaandaa mafunzo baada ya kufanya utafiti wa kujua mahitaji kwa wadau mbalimbali na malengo ya mafunzo hayo ni kuimarisha utendaji kazi katika ngazi zote za elimu kuanzia shuleni, katika kata, halmashauri, mkoa na wizara,”alisema .

Na kuongeza “Malengo mengine ni kuimarisha usimamizi wa utoaji wa elimu bora shuleni kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na miongozo ya elimu, kuziba ombwe la maarifa na ujuzi ambalo kiongozi au mtendaji hakupata katika mafunzo ya awali ya Ualimu na kuongeza idadi ya viongozi wenye maarifa ya uongozi na usimamizi wa elimu,”alisema Dkt Mgullah

Alisema Katika kipindi cha miaka mitano (2018- 2022), Wakala umetoa machapisho ya Moduli ya wajibu na majukumu ya Mjumbe wa Kamati na Bodi ya Shule,

Wajibu na majukumu ya Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Ualimu 2022

Alibainisha kuwa ,Moduli ya udhibiti ubora wa Shule wa ndani 2021 na uandaaji na usimamizi wa Utekelezaji wa Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Shule - 2018