Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 1:29 pm

NEWS: WAJERUMANI WALIA NA MAKALI YA NISHATI NA VYAKULA

Bon. Wananchi nchini Ujerumani wameanza kuhisi makali ya maisha mara baada ya ongezeko kubwa la bei ya umeme, nishati na vyakula kwa ujumla, ikiwa ni athari ya vikwazo dhidi ya Urusi.

Hali ilivyo kwasasa Ujerumani Kadri mfumuko wa bei unavyoongezeka ndivyo watu wanavyozidi kutoridhishwa na serikali yao. Hayo yanajiri huku serikali ikitangaza hatua za kupunguza matumizi ya nishati kote nchini.

Usafiri umekuwa ghali nchini Ujerumani tangu Septemba mosi. Katika miezi ya Juni, Julai na Agosti, kodi ya nishati ilipunguzwa. Aidha usafiri wa umma uligharimu euro tisa pekee kila mwezi. Lakini sasa bei ya mafuta imepanda ghafla, huku nauli kwenye treni na mabasi zikirudi kama zilivyokuwa awali. Na kana kwamba masaibu hayo hayaishi, kuna uwezekano nauli zitaendelea kuongezeka kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta.

Wakati huo huo, kampuni za gesi na umeme zinazidi kuwatumia wateja wao taarifa kuhusu ongezeko la bei ya bidhaa hizo.

Swali kuu ambalo wengi wanajiuliza na ambalo limetawala mijadala ya umma hata kuwa ajenda ya kisiasa ni je, hali itakuwaje?