Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 3:18 pm

NEWS: URUSI YATANGAZA KUFANYA SHEREHE YA KUNYAKUWA MAENEO YA UKRAINE

Ikulu ya rais wa Urusi Vladimir Putin, imetangaza kuwa taifa hilo litayachukuwa rasmi maeneo manne ya Ukraine yanayokaliwa na vikosi vyake.

Hatua hiyo itatangazwa katika sherehe kubwa hapo kesho Ijumaa mjini Moscow na kutishia kuwa itatumia silaha za nyuklia kutetea maeneo hayo.

Vladimir Putin News, Video & Photos | NBC News

Msemaji wa rais wa Urusi Vladimir Putin, Dmitry Peskov, amesema hafla ya kutwaa rasmi maeneo hayo itaandaliwa katika ikulu hiyo ya Kremlin na kuongeza kuwa rais huyo atahutubia taifa.

Peskov amewaambia wanahabari kwamba kesho Ijumaa hafla hiyo ya kutiwa saini ili kujumuishwa kwa maeneo hayo itafanyika katika ukumbi wa Mtakatifu George katika ikulu ya Kremlin majira ya saa tisa mchana.

Viongozi wanne wa maeneo yanayokaliwa na Urusi nchini Ukraine na wanaoungwa mkono na Urusi, waliwasili leo hii nchini Urusi, baada ya kumtaka Rais Vladimir Putin kuyanyakua rasmi maeneo hayo.