Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 9:09 am

NEWS: URUSI YASHAMBULIA GRIDI YA UMEME YA TAIFA YA UKRAINE

Jeshi la Urusi limeshambulia vikali gridi ya taifa ya umeme ya Ukraine katika mwa nchi hiyo jana usiku na kusababisha kitisho kikubwa cha changamoto zaidi ya usambazaji wa nishati hiyo na hii ni kulingana na mwendeshaji wa gridi hiyo ya Ukrenergo mapema leo.

Russia Ukraine update: Explosions rock Kyiv a week after strikes

Amesema kwenye taarifa kupitia Telegram kwamba kumekuwepo na uharibifu wa vifaa katika mtambo huo mkubwa kabisa wa mifumo ya usambazaji umeme katika maeneo ya katikati mwa Ukraine. Urusi imeongeza mashambulizi kwenye miundombinu muhimu ya Ukraine ikiwa ni pamoja na mitambo ya umeme katika wiki za karibuni na kuwaacha mamilioni wakikosa umeme na mifumo ya joto kwa muda mrefu wakati majira ya baridi yakikaribia.