Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 8:34 am

NEWS: ULAYA KUIPA URUSI HADHI YA TAIFA LINALOFADHILI UGAIDI

Wabunge wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa leo kuipa Urusi hadhi ya taifa linalodhamini ugaidi kutokana na matendo ya nchi hiyo katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Itakuwa mara ya kwanza kwa Umoja wa Ulaya kwa ujumla wake kuchukuwa hatua kama hiyo, lakini haijulikani itakuwa na maana gani. Uamuzi huo umefikiwa kufuatia rai ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy.

Size of Parliament to shrink after Brexit | News | European Parliament

Kulingana na waraka ulioandaliwa na idara ya utafiti ya Bunge la Ulaya, Urusi inayaelekeza mashambulizi yake kuwalenga raia na miundombinu ya kiraia, ikiwemo hospitali, shule na vituo vya afya.

Wachambuzi wanasema ikiwa Bunge la Ulaya litapitisha azimio hilo litakuwa ishara ya kulaani matendo ya Urusi nchini Ukraine na nje ya nchi hiyo.

Hadi sasa Marekani inajizuia kuichukulia Urusi hatua kama hiyo, kwa hoja ya kuzuia athari zisizokusudiwa katika mfumo wake wa sheria.