Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 12:21 pm

NEWS: TFF YAMEPEWA SIKU 21 NA SEREKALI UDHAMINI WA GSM

Dar es saalm.Tume ya Ushindani nchini (FCC) imelipa siku 21 Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kulitatua sakata la udhamini wa kampuni ya GSM na club za ligi kuu.

FCC imetoa agiza hilo baada ya kuibuka kwa mvutano kuhusu mkataba huo hivyo TFF inatakiwa ipeleke taarifa muhimu za mikataba.

Hayo yamebainishwa Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari iliyoandaliwa na FCC leo jijini Dar es Salaam.

Urio amesema suala la GSM linashughulikiwa, TFF imepewa siku 21 kupeleka taarifa zote muhimu na tayari wameanza kupeleka.

Juzi Desemba 17 Shirikisho hilo la Soka kupitia bodi ya ligi lilifanya kikao na wenyeviti wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine kilitoka na azimio la kukubali Kampuni ya GSM kuendelea kuwa mdhamini mwenza wa ligi kuu Tanzania bara.

Taarifa ya kikao hicho ambacho kilishirikisha timu zote kilisema kuwa vilabu 15 kati ya 16 viliridhia makubaliano ya GSM na kuliomba shirikisho la Soka TFF pamoja na bodi ya ligi kuendelea kutafuta wadhamini wengine zaidi.