Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:16 am

NEWS: RAIS MUSEVEN AMPANDISHA CHEO MWANAE KUWA JENERARI KAMILI

Rais wa Uganda Yoweri Museven amemwondoa mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kwenye wadhifa wa kamanda wa jeshi la nchi kavu na wakati huo huo kumpandisha cheo kuwa jenerali kamili.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameshikilia wadhifa wa kamanda wa jeshi la nchi kavu kwa muda wa miaka miwili na mojawapo ya operesheni maarufu alizoongoza ni ile ya shujaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rise of Ugandan leader's son draws excitement and concern | The Seattle Times

Kamanda wa operesheni hiyo meja jenerali Kayanja Muhanga ndiye amechukua nafasi hiyo sasa kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa Jumanne alasiri.

Haijafahamika kama rais Yoweri Museveni amechukua hatua ya kumwondoa mwanawe kwenye wadhifa wa kamanda wa jeshi la nchi kavu baada ya yeye kusambaza ujumbe ulioshtumiwa na raia wengi wa Kenya na Uganda kwenye mitandao ya kijamii.

Ujumbe huo umeibua hisia mseto za hasira na kejeli kutoka kwa raia wa nchi hizo mbili, wakati rais William Ruto wa Kenya akitarajiwa kufanya ziara rasmi Uganda wiki hii.

Katika mfululizo wa ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa tweeter, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mtoto wa rais Museveni amesambaza taarifa ambazo zinagusia ubabe wa kijeshi ilio nao Uganda dhidi ya Kenya na pia kuhusu dhana ya mageuzi ya kisiasa anayoamini inaweza kuzifanya nchi hizi mbili kuwa nchi moja katika muda wa wiki mbili tu.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Uganda imelazimika kuwasilisha taarifa ya kuomba radhi kutoka kwa ile ya Kenya ikisisitiza kuwa ujumbe huo ni maoni ya mtu binafsi wala si msimamo wa taifa la Uganda.

Kinaya cha kumwondoa jenerali huyo kwenye wadhifa wa kamanda wa jeshi la nchi kavu na kisha kumpandisha cheo kimeibua mitazamo kwamba sasa atakuwa na uhuru wa kujishughulisha na siasa bila kuvunja sheria za kijeshi.