Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:46 am

NEWS: MWANAFUNZI AJIUA KWA RISASI, ATAKA MWILI WAKE KUCHOMWA

Moshi. Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari St Mary Goreti iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Robert Meier (17) amejiua kwa kujipiga risasi huku akiacha ujumbe akitaka mwili wake uteketezwe na moto na Majivu yake yapelekwe Marakani.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema lilitokea usiku wa kuamkia juzi.

Kamnada Maigwa amesema kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kujiua, aliacha ujumbe wa maandishi ulisomeka mwili wake uchomwe na majivu yake yasafirishwe kwenda Marekani yakazikwe pembezoni mwa kaburi la baba yake.

Kwa mujibu wa Kamanda Maigwa, baba yake Robert alifariki dunia akiwa Marekani na mwili wake ulizikwa nchini humo.

Kamanda Maigwa alifafanua kuwa siku ya tukio saa 8 usiku wa kuamkia juzi huko Mwereni katika Kata ya Ngangamfumuni, mwanafunzi huyo alijiua kwa kujipiga risasi kifuani upande wa kushoto kwenye moyo na risasi hiyo ikatokea mgongoni.

Alisema alijiua kwa kwa kutumia bastola namba LXE 023 aina ya Glock iliyotengenezwa nchini Austria, inayomilikiwa kihalali na mtu aitwaye Boniface Kimario, mkazi wa Mwereni ambaye Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano zaidi.