Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 2:26 pm

NEWS: MWAKYEMBE AWAPONGEZA AY NA MWANA FA KUIBURUZA TIGO MAHAKAMANI

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dk Harrison Mwakyembe amewapongeza wasanii wa kizazi kipya(Bongofleva), Ambwene Yessaya ‘AY’ na Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ baada ya kupata ushindi kwenye kesi yao ya madai dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya nchini Tanzania Tigo.

Image result for AY na mwana fa

Dkt Mwakyembe amesema hayo leo Jumatano Agosti 28,2019 katika mkutano aliouitisha akiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa lengo la gawio la miraba kwa wanamuziki wa dansi

Image result for AY na mwana fa

Mkutano huo pia lengo lake ni kuunganisha Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Bodi ya Filamu na Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) ili kuboresha huduma za sanaa na hakimiliki.

Amesema amefurahishwa wasanii hao kupigania haki yao na kuipata hivyo ndivyo inavyotakiwa kwa wasanii wote wa Tanzania.

Mahakama ya Tanzania iliiamuru kampuni ya mawasiliano ya Tigo iwalipe wasanii hao Sh2.1 bilioni kwa kutumia nyimbo zao (Usije Mjini, Dakika Moja) bila idhini yao.