Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 2:55 pm

NEWS: MTU MMOJA AWAPIGA RISASI WANAFUNZI 6 NCHINI URUSI

Mtu mwenye silaha amefyatua risasi hovyo katika shule moja nchini Urusi, na kufanikiwa kuua takriban watu sita huku akijeruhi ishirini.

Shambulizi hilo lilifanyika katika shule nambari 88, ikiwa na karibu wanafunzi 1000 na walimu 80.

Mshambuliaji huyo ameripotiwa kujiua na chanzo cha kufyatua risasi hakijafahamika.

7 Children killed in shooting at a Russian school - ZambiaNews365.com

Katika chambulio hilo Waathiriwa ni pamoja na wanafunzi wa shule hiyo na mlinzi wa shule katika jiji la Izhevsk.

Vyombo vya habari vya Urusi vimechapisha video mtandaoni ambazo zinaonekana kurekodiwa ndani ya shule ambayo shambulizi lilitokea.

Several children killed in Russia school shooting | Gun Violence News | Al Jazeera

Video moja inaonekana kuonyesha damu sakafuni na tundu ambalo risasi ilipita kwenye dirisha, huku watoto wakiinama chini ya madawati.

Mshambuliaji huyo aliripotiwa kuwa na bastola mbili, kulingana na mbunge wa jimbo aliyenukuliwa na shirika la habari la Tass.

Shule hiyo iko katikati mwa Izhevsk, jiji lenye wakazi wapatao 650,000, karibu na majengo ya serikali kuu.

Walimu na wanafunzi wamehamishwa.