Home | Terms & Conditions | Help

May 4, 2024, 5:47 pm

NEWS: MIILI YA WATOTO WALIONYOFOLEWA MACHO NA KUCHUNWA GOZI WAZIKWA

Tabora. Hatimaye Watoto mapacha waliozaliwa kabla ya wakati na mmoja wao kunyofolewa jicho na ngozi ya paji la uso wakiwa Kituo cha Afya Kaliua, miili yao imezikwa kimila ndani ya nyumba katika kijiji cha Kalemela Wilayani Urambo Mkoani Tabora.

Baba wa watoto hao Bw. Isaka Rafael (27), amesema tayari miili ya Watoto wake imezikwa lakini ameiomba Serikali kusimamia haki ya Watoto wake Mahakamani na kuhakikisha kila aliyehusika anapata adhabu inayostahili.

Isaka ameishukuru pia Serikali, Wadau na Wananachi wote kwa ushirikiano alioupata tangu sakata hilo lilipoibuliwa.

Kwa upande wake RC Tabora ameendelea kusisitiza kuwa Wauguzi wanne wa Kituo cha Afya Kaliua watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili wakati wowote kuanzia sasa kuhusiana na sakata hilo.