Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 12:42 pm

NEWS: MBATIA AFUKUZWA RASMI NCCR MAGEUZI

Dodoma. Chama cha NCCR Mageuzi kupitia Mkutano mkuu wa Chama hicho uliofanyika hii leo Jumamosi kimemtimua na kumvua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia na kumvua uongozi Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Angelina Rutairwa.

Aidha, mkutano huo ulitaka viongozi wote waliohusika na ubadhilifu wa mali akiwemo Mbatia kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mkutano huo umefanyika hii leo Jumamosi Septemba 24, 2022 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe 224 kati ya 368 waliopo kwa mujibu wa Katiba ya chama chao.

Hatua ya wajumbe wa NCCR kumvua Uwanachama Mbatia Imekuja mara baada ya Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Haji Ambari Hassan kutaja tuhuma saba zinazomkabili Mbatia na tuhuma mbili za Angelina.

Miongoni mwa tuhuma hizo Mbatia ni kuuza mali za chama, ikiwemo mashamba na nyumba katika maeneo mbalimbali.

Ambari amewaambia wajumbe hao kuwa viongozi hao walipelekewa hati ya mashtaka yao na walitakiwa kujibu ndani ya siku 14 kama katiba yao inavyotaka.

Hata hivyo, amesema kuwa hakujibu mshtaka hayo na wala hakufika katika mkutano huo licha ya kualikwa ili aweze kujitetea mbele ya wajumbe.

"Tumewaita katika mkutano huu lakini hawakutaka kuja na badala yake walikimbilia mahakamani kuzuia kwa mara nyingine mkutano huo.

Aidha, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini ya chama hicho Joseph Selasini amesema halmashauri kuu ya chama hicho imewatimua uanachama wanachama 10 kwa utovu wa nidhamu uliokidhiri akiwemo Edward Simbeye.