Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 2:55 pm

NEWS: MAHAKAMA YA JUU KENYA IMESEMA ITATOLEA UWAMUZI MAMBO TISA

Nairobi. Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya hatimaye imeanza kusikiliza Kesi za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022 na kufanya tathmini masuala mbalimbali yatakayoshughulikiwa kwenye kesi zilizowasilishwa kupinga kutangazwa kwa William Ruto kuwa Rais Mteule.

Jaji mkuu Martha Koome ameyataja mambo 9 ambayo mahakama hiyo itafanya uamuzi kuyahusu baada ya kuziunganisha baadhi ya kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi huo .

Mambo hayo tisa ni kama yafuatayo;
1.Iwapo teknolojia iliyotumiwa katika uchaguzi na Tume huru ya uchaguzi na Mipaka IEBC iliafikia viwango vya ubora wa hadhi kuwezesha uchaguzi unaoweza kuthibithitishwa na ulio salama kwa lengo la kutoa matokeo sahihi na yanayoweza kuthibitishwa.

2.Iwapo kulikuwa na aina yoyote ya kuingilia jinsi fomu 34A zilivyopakuliwa na kuwasilishwa kwa tovuti ya IEBC .

3.Iwapo kulikuwa na tofauti kati ya fomu 34A zilizopakuliwa katika tovuti ya IEBC zilizowasilishwa kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura na zilizopewa mawakala katika vituo vya kupiga kura.

4.Iwapo kuahirishwa kwa chaguzi za ugavana katika kaunti za Kakamega na Mombasa na maeneo bunge manne Pamoja na wadi mbili kulikuwa ni kubana idadi ya wapiga kura waliojitokeza kupiga kura na kuathiri mlalamishi mkuu ambao ni Raila Odinga na Martha Karua .

5. Iwapo kulikuwa na tofauti isiyoeleweka kati ya kura za urais na za nyadhifa nyingine .

6.Iwapo Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ilifanya uthibitisho ,ujumlishaji na kwa mujibu wa sheria.

7.Iwapo rais mteule William Ruto alipata asilimia 50+1 ya kura zote zilizopigwa kwa mujibu wa katiba ili kutangazwa mshindi .

8.Iwapo kulikuwa na kasoro katika idadi hiyo kuathiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

9.Na Maelekezo ya mahakama ya Juu Zaidi kuhusu kesi hizo .

Kikao cha kabla ya kesi kinaendelea na Malalamiko mawili yamefutwa. Mahakama iliacha maombi 7 ya kuzingatiwa na yote yaliunganishwa kwa sababu yanaibua masuala yanayofanana na kutaka amri zinazofanana.