Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:25 am

NEWS: LIFT YAANGUKA MILLENIUM TOWER DAR

Dar es salaam. Watu saba wamenusurika kifo baada ya lifti kuanguka kutoka ghorofa ya 10 katika jengo la refu la Millenium Tower lililopo Kijitonyama Jijini Dar es salaam, majeruhi hao wamepelekwa katika Hospitali ya jirani ya Kairuki kwa ajili ya matibabu.

Kwamujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania limesema chanzo ni lifti hiyo iliyokuwa imebeba zaidi ya Watu kumi kuzidiwa uzito

“lifti ilizidiwa uzito na ilikuwa imefanyiwa matengenezo hivi karibuni ambapo leo ilikuwa inajaribiwa na kulikuwa na Fundi ndani” Askari wa Zimamoto na Uokoaji Inspekta Msaidizi Mohammed kutoka Kinondoni amesema kilichofanywa na Uongozi wa jengo hilo lenye ghorofa 25 ni makosa kwa kuwa hawakupaswa kufanya majaribio ya lift kukiwa na Watu ndani bali walitakiwa kuweka kitu chochote chenye uzito ndani ya lifti ndio waifanyie marekebisho.

Hata hivyo uongozi wa Jengo hilo lenye zaidi ya gorifa 20 hawajasema chochote na badala yake wameomba kupewa muda ili waje na majibu sahihi.