Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 11:46 am

NEWS: KATIBU WA WANAWAKE CHADEMA ACHILIWA HURU

Musoma. Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Bi Catherine Ruge ameachiliwa huru kwa dhamana Usiku wa kuamkia leo Jumapili na Jeshi la Polisi mkoani Mara baada ya kushikiliwa kwa mahojiano kwa saa kadhaa.

Ruge alikamatwa Jana mchana siku ya Jumamosi Septemba 24, 2022 alipofika kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari juu ya msimamo wa familia za watu watatu waliouawa kwa kupigwa risasi na askari polisi wilayani Serengeti kwa tuhuma za kuhusika na ujambazi.

Waliouawa katika tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Septemba 23, 2022 ni Mairo Togoro (56), mkazi wa kijiji cha Majimoto, Mwise Simon (54) mkazi wa kijiji Nyamihuru na Mugare Mokiri mkazi wa kijiji cha Nyamikobiti wote wa wilaya ya Serengeti ambaye ni mjomba wake, Ruge.

Polisi walidai watu hao walikamatwa kwenye operesheni iliyofanywa kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, Mwanza, Simiyu na Kanda maalumu ya Tarime/Rorya kufuatia matukio ya ujambazi wa kutumia silaha, matukio yanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa hao wakishirikiana na wenzao ambao hawakutajwa.

Akizungumza kwa njia ya simu, Ruge amesema kuwa ameachiwa usiku wa kuamkia leo kwa dhamana na kutakiwa kuripoti polisi Jumatatu.

"Nimejidhamini mwenyewe tena bila hata ya kutoa kitambulisho wameniambia niripoti Jumatatu," amesema.

“Nimeachiwa baada ya kuandika maelezo ya Onyo na kujidhamini mwenyewe"Kosa la Uchochezi"

Najua hii ni Intimidation ya Polisi ila sitarudi nyuma. Mapambano yanaendelea” aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitte

Amesema baada ya kukamatwa, alipelekwa ofisini kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara (RCO) kwa ajili ya mahojiano ambayo yalidumu kwa saa kadhaa.
Mazungumzo ya polisi yalikuwa ya kunituhumu kwa kufanya uchochezi kwa jamii