Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 10:07 am

NEWS: ITAMGHARIMU ODINGA MILIONI 30 KUFUNGUA KESI KUPINGA MATOKEO

Nairobi. Itamgharimu aliyekuwa Mgombea wa Urais wa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga, kiasi cha zaidi ya Sh 30 milioni kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya urais katika Mahakama ya Juu nchini humo.

Kiongozi huyo wa ODM anatazamiwa kuwasilisha kesi yake ya kupinga ushindi wa mpinzani wake William Ruto aliyetangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na mipaka (IEBC) Jumatatu hii kama Rais Mteule wa Taifa la Kenya.


IEBC kupitia Mwenyekiti wake Wafula Chebukati ilimtangaza Ruto kama Rais Mteule, mara baada ya kupata Kura 7,176,141 sawa asilimia 50.5 ya kura zote huku Mpenzi wake Raila Odinga akipata kura 6,942,930 sawa na asilimia 48.8

Matokeo ya mwisho kutoka IEBC

WagombeaKura
Willim Rut

50.5%

Kura za Ruto7,176,141
Raila Odinga

48.8%

Kura za Odinga6,942,930
Wagombea wengine

0.6%

Kura za wagombea wengine93,956


Ushindi wa Bw. Rutto Ulighubikwa sintofahamu nyingi mara baada ya tume yenyewe ya uchaguzi kugawanyika vipande viwili. Makamishna wanne kati ya saba wa tume hiyo ya uchaguzi wakiongozwa na Naibu Mwenyekiti Juliana Cherera waliyapiga matokeo hayo muda mchache kabla ya Bw Chebukati kumtangaza Ruto kama mshindi wa Uchaguzi.

"Hatuwezi kubeba dhima ya matokeo yatakayotangazwa, kwa sababu ya ukosefu wa uwazi katika awamu hii ya mwisho ya uchaguzi mkuu," alisema. Bi Cherera. Tume ya Uchaguzi inao ma kamishna saba tu.

Kulikuwa na matukio ya fujo ndani ya kituo kikuu cha kuhesabia kura. Mizozo ilizuka jukwaani huku mkuu wa tume hiyo Wafula Chebukati akionekana kukaribia kutangaza matokeo.

Bw Chebukati baadaye alirejea kumtangaza Bw Ruto kuwa mshindi, na kusisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Matokeo rasmi yanaonyesha kuwa Bw Ruto alijiimarisha katika ngome za Raila Odinga, mpinzani wake mkuu. Pia alishinda kwa kishindo katika eneo la Mlima Kenya - kitovu cha kisiasa cha mgombea mwenza wa Bw Odinga Martha Karua na Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta.

Hii ilisaidia kurahisisha uchaguzi kwa upande wa Bw Ruto.

Alikuwa ni mtu 'duni' au, kama alivyopendelea kujiita, "hustler", akipambana na kile alichokiona kama jaribio la nasaba mbili kubwa za kisiasa za Kenya - Odingas na Kenyattas - kusalia madarakani. Simulizi hii iliwagusa vijana wengi wa Kenya.

Ruto mwenye umri wa miaka 55 alikuwa nyuma ya Odinga katika kura za maoni, na akakabiliana na mpinzani mkubwa - Bw Odinga - ambaye, katika hali isiyo ya kawaida, aliungwa mkono na mpinzani wake wa muda mrefu, Rais Kenyatta.

Rais sasa atalazimika kukubali kilichotokea na kukabidhi hatamu za uongozi kwa naibu wake - mtu ambaye alimtaja wakati wa kampeni kuwa "haaminiki".