Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 4:21 pm

NEWS: FIFA NA UEFA ZAIFUNGIA URUSI KWA MUDA

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA na la barani Ulaya, UEFA yametangaza jana kuzisimamisha timu za taifa la Urusi kushiriki michuano yake yote hadi taarifa nyingine itakapotolewa.

Hatua hii inachukuliwa baada ya Poland, Sweden na Jamhuri ya watu wa Czech kukataa kucheza dhidi ya Urusi. Mashirikisho hayo yamesema kwamba kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, hawana budi kuvisimamisha vilabu vyote vya Urusi pamoja na timu ya taifa.

Hatua hiyo ambayo hata kama itatekelezwa kwa muda mfupi huenda ikaiengua Urusi kwenye michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwakani nchini Qatar na timu yake ya wanawake kushiriki michuano ya wanawake ya Euro nchini Uingereza mwezi Julai.