Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 2:27 pm

NEWS: DIAMOND ASHINDA TUZO YA AFRIMMA 2021

Dar es salaam. Staa wa Muziki wa label ya WCB kutoka nchini Tanzania Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ametwaa tuzo ya Mwanamuziki bora wa mwaka wa kiume kwa Afrika Mashariki katika tuzo za AFRIMMA 2021.

Diamond ameshinda tuzo hiyo kwa kuwapiku wanamuziki Ali Kiba kutoka Tanzania, Eddy Kenzo kutoka Uganda, Ben kutoka Rwanda, Khaligraph Jones kutoka Kenya, Gildo Kassa kutoka Ethiopia, Otile Brown kutoka Kenya na Meddy kutoka Rwanda.

Aidha Tuzo kwa mwanamuziki bora wa kike Afrika Mashariki imeenda kwa Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ambapo alikuwa akishindanishwa na Nadia Mukami kutoka Kenya, Vinka kutoka Uganda, Zuchu kutoka Tanzania, Sheebah Karungi kutoka Uganda, Nikita Kering kutoka Kenya, Tanasha Donna kutoka Kenya na Knowles Butera kutoka Rwanda.

Kwa video bora ya mwaka ya AFRIMMA, ameshinda Flavour ft Diamond Platnumz x Fally Ipupa (Berna) ambapo alikuwa akishindanishwa na Tay C (Le Temps), Teni (Hustle), Mz Vee (Bosi Mbaya zaidi), Zuchu (Sukari), Ray Vanny x Innos’B (Kelebe), Rema (Bounce) na Wizkid ft Tems (Essence).

Mwongozaji bora wa Video ameshinda Director Kenny kutoka Tanzania ambapo alikuwa akishindanishwa na Dkt. Nkeng Stephens kutoka Cameroon, Deska Torres kutoka Kenya, TG Omori kutoka Nigeria, David Duncan kutoka Ghana, Sasha Vybz kutoka Uganda, Dammy Twitch kutoka Nigeria na Ofntse Mwase kutoka Afrika Kusini.