Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 2:08 pm

MKUTANO WA ACT WAPIGWA STOP TUNDURU

Jeshi la Polisi Mkoani Tunduru Limempiga marufuku Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu kufanya ziara mkoani humo kwa madai ya Matishio ya ugaidi nchini.

Katazo hilo lemetolewa usiku wa kuamkia leo Octoba 4,2022 na Kamanda wa Polisi Tunduru.

Kufuatia katazo hilo chama cha ACT Wazalendo kimelitaka Jeshi la Polisi nchini kueleza umma kinagaubaga juu ya hatari hiyo ya kiusalama

“Tunalitaka Jeshi la Polisi liueleze Umma juu ya Ugaidi huu maana ni hatari kwa usalama wa Raia” amesema Doroth Simu Makamo Mwenyekiti wa ACT Wazalendo bara.

“Bwana IGP Wambura @tanpol kuna tishio la Ugaidi nchini? Level gani? Tishio hili limetangazwa lini? Kwa hiyo watalii wasiende Selous au sio? Huyu OCD Tunduru amepata idhini yako kutangaza tishio la Ugaidi? Mnawezaje kuthubutu kuzuia Ziara ya Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo?” Amehoji Zitto Kabwe Kiongozi Mkuu wa Chama hich

Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Goodbless Lema amelaani vikali hatua hiyo ya Polisi na kusema kuwa hatua hiyo itadhoofisha juhudi za Rais kwa wawekezaji na watalii nchini.

“Sijui kama mnajua thamani ya huu ujinga unavyo chafua Nchi na kuongeza wasiwasi kwa wawekezaji. Mnanadi utalii…… halafu mnatangazia Dunia kuwa Tanzania kuna ugaidi? ili mpate sababu ya kuminya demokrasia? Mwisho wa ujinga ni mauti” amesema Lema