Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 8:47 am

Magufuli awatumbua maafisa wa serekali mkoani Kagera

Rais Dr. John Magufuli amewafukuza kazi maafisa watatu wa serekali kwa tuhuma za kutaka kupora pesa za wahanga wa tetemeko la Ardhi kagera


Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Steven Makonda.

Taarifa kutoka ikulu imesema kiongozi huyo amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine kwa jina "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha.

Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Rais kupokea msaada wa Shilingi milioni 545 kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi za kusaidia waathiriwa wa tetemeko hilo la ardhi lililotokea 10 Septemba, 2016.

Bw Majaliwa ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya "Kamati Maafa Kagera".