Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 7:34 am

KOREA YA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA LENYE UWEZO WA KUFIKA MAREKANI

Taifa la Korea ya Kaskazini mapema leo Alfajiri limefanya jaribio la kombora la masafa marefu lenye uwezo wa kufika nchini Marekani kufuatia tishio hilo Korea Kusini na Marekani leo zimefanya luteka ya pamoja ya kijeshi zikitumia ndege za kivita chapa F-35A kujibu jaribio la kombora la masafa marefu la Korea kaskazini.

North Korea claims 'new tactical guided' missiles launched - BBC News

Taarifa ya luteka hiyo imetolewa na wizara ya ulinzi ya Korea Kusini saa chache baada ya Pyongyang kufyetua kombora ambalo lilianguka karibu na eneo la bahari ya Japan. Maafisa mjini Tokyo wamesema kombora hilo ambalo sehemu ya jaribio la pili kufanywa na Korea Kaskazini ndani ya mwezi Novemba lina uwezo wa kuifikia Marekani.

With ICBM launch, Japan sees dramatic shift in North Korean missile testing | The Japan Times

Jaribio hilo limezusha ukosoaji mkubwa wa kimataifa. Viongozi wa Marekani, Korea Kusini, New Zealand, Japan na Australia walifanya kikao cha dharura hii leo ambapo wamelaani kwa matamshi makali jaribio hilo na mpango mzima wa silaha nzito wa Koea Kaskazini.