Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 3:53 pm

BURUDANI: USHAURI WA DIAMOND KWA WASANII WENZAKE

Mwanamuzi staa wa Bongo flevani nchini Tanzania Naseeb Abdul, maarufu kama ‘Diamond Platnumz’ amewataka wasanii wenzake kutumia vivutio vya Taifa katika kazi zao ili kutangaza utalii uliopo nchini.

Tokeo la picha la diamond platnumz

Diamond Platnumz amejisema kwa upande wake binafsi yupo tayari kutangaza vivutio mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza nchi yake kupitia kazi zake.

“Haiwezekani mastaa kutoka nchi zingine kutembelea vivutio vyetu wakati sisi wenyewe tupo karibu na tunashindwa kwenda, mastaa wengi wamekuja nchini kama vile David, Beckham, Lionel Messi wamepanda mlima wetu Kilimanjaro.

Tokeo la picha la diamond platnumz mlima kilimanjaro

“Nimefurahi kupanda Kilimanjaro japokuwa sikufanikiwa kufika kileleni, lakini kwangu ni jambo la kubwa na historia, hivyo wasanii kupitia kazi zetu inabidi tutangaze vivutio vyetu ili watalii waje, nchi ijulikane na tukuze uchumi wetu,” alisema msanii huyo.