- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
Zitto Kabwe: "Yanayo endelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu"
Dar es salaam: Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo na Mbuge wa Kigoma Mjini/ujiji Mh. Zitto Zuberi Kabwe ameonya dhidi ya yale yanayo endelea katika nchi yetu hasa tabia ya watu na viongozi kushabikia kitendo ya Mwenyekiti wa Yanga Africa na Mmiliki wa kampuni ya Quality group Bwana Yusuph Manji kwamba ni ya Manji pekee yake na kana kwamba hayata wafikia.
akiandika kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto amesema kuwa "Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wenyewe." alisema kuwa "Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha. Ila Manji azikose tu. Pia Zitto akahoji mfumo ulio tumiwa kufreezi sakata la Escro "Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku. Leo mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow?"
Zitto anasema Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20% kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia hisa kutoka nje ya Tanzania wanahangaika na Mtanzania aliyezirudisha hisa Tanzania.
Pia Zitto akazungumzia swala la ofisi ya uhamiaji Kumtaka maji ajibu Tuhuma za kuajiri watu wasio na vibali "Uhamiaji wanamwita kuhusu wafanyakazi wake wageni kana kwamba yeye Yusuf ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni. Aliko Dangote hakuitwa uhamiaji kwa suala la wafanyakazi wake ila Manji anaitwa.
Wakifanikiwa kwa Manji atatafutwa mwengine, Ni sawa na kula nyama ya mtu. Hutaacha.
Manji anaweza kuwa ana madudu mengi Sana, ahukumiwe kwa haki kwa makosa yake. Asikomeshwe kwani ukomeshaji hautaishia kwake. Asionewe. Atendewe haki.
Zitto akawasihi wanachama wa Yanga kwa kusema "nawasihi Yanga achaneni na mambo ya mabango uwanjani. Hayasaidii lolote"