- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
ZITTO: HOJA YA TZS 1.5 TRILIONI HAIWEZI KULALA FOFOFO, HAIJAPATIWA MAJIBU
Dar es salaam: Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amerejesha tena sakata la upotevu wa pesa za wananchi TZS 1.5 Trilioni zilizoripotiwa Kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serekali (CAG) kwa mwaka 2016/2017 ambayo ilitolewa March 30 mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi.
Kupitia Ukurasa wake wa Twitter Leo June 4, 2018 Zitto amesema kuwa hoja ya Upotevu wa pesa TZS 1.5 Trilioni haiwezi kulala fofofo kwa sababu hoja hii Haijapatiwa majibu Sahihi
"Serikali ilipiga porojo na kutisha wakosoaji tu. Hatua stahiki ni Spika wa Bunge kuruhusu ukaguzi Maalumu na Taarifa kuwasilishwa Bungeni. Serikali ya Rais ya Rais Magufuli inafilisi nchi yetu" amesema Zitto
Zitto aliwahi kuuliza Maswali muhimu katika Ripoti ya CAG 2016/17 kutoka kwa Serekali ya Rais Magufuli
- Zipo wapi Shilingi Trilioni 1.5 zilizokusanywa na Serikali Lakini hazikutolewa kwa matumizi wala kukaguliwa? Ukurasa 34
- Kwanini Serikali imekopa TZS 500 bilioni zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge. Uk 30
- Kwanini Serikali imetekeleza 68% tu ya Bajeti ya Maendeleo kwa Serikali Kuu na 51% tu kwa Serikali za Mitaa? uk 38
- Kwanini Serikali ilitumia zaidi ya shilingi 219 bilioni, kulipa madeni ya nyuma ambayo hayakuwa kwenye Bajeti? uk 40
- Kwanini Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wametoa Takwimu za Uongo za Mapato ya Kodi ya zaidi ya shilingi 2.2 trilioni? uk 109
- Serikali ya Jamhuri ya Muungano imepata Hati Chafu ( Hesabu Jumuifu za Taifa ). Kwanini Katibu Mkuu Hazina hajachukuliwa hatua kama ilivyokuwa kwa Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa? uk 296-29
Nayo Kwa upande wa serekali Naibu waziri wake wa Fedha Ashantu kijaji ilijibu hoja hiyo kwa kusema kuwa kiasi cha Sh697 bilioni kilitumika katika matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva, Sh 687bilioni kwa ajili ya mapato tarajiwa na Sh 203 bilioni ni za mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar.
Kutolewa kwa majibu hayo na Naibu Waziri, kulikuja baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kukatisha kipindi cha maswali na majibu na kuipa serikali nafasi ya kutoa hoja ya kutoonekana kwa Sh 1.5 trilioni kwenye matumizi ya Serikali.
“Hakuna Fedha kiasi cha Sh1.5trilioni iliyopotea au kutumika kwenye matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Bunge tukufu. Madai ya watu wasiyoitakia mema nchi kuhusu matumizi ya fedha hii hawana nia njema na nchi,”amesema Dk Kijaji
Amesema kutoonekana kwa fedha hiyo kulitokana na taarifa ya ukaguzi ya CAG kutumia taarifa za hesabu za nyaraka mbalimbali na hivyo kutojumuishwa kwa baadhi ya taarifa za utekelezaji wa bajeti.
Amesema hadi kufikia Juni 2017, mapato yalikuwa Sh 25.3 trilioni na matumizi yalikuwa Sh23.79 trilioni.
“Matumizi haya hayakujumuisha Sh 697.85bilioni zilizotumika kulipa dhamana na hati fungani za serikali zilizoiva,” amesema
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kuwa katika ukurasa wa 34 wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali, (CAG)Sh 1.5 trilioni hazikutolewa kwa matumizi wala kukaguliwa.