Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:35 pm

Wanaume [mafataki] waonywa na DC Gondwe

TANGA; Pamoja na juhudi za serikali kupambana na kutokomeza swala la watoto kukatisha masomo yao kwa sababu zisizokuwa za msingi . Godwin Gondwe ambaye ni mkuu wa wilaya ya handeni mkoani Tanga ametoa onyo kwa wanaume wanao wadanganya wanafunzi wa kike pamoja na wazazi wanao wakatisha watoto wao masomo kuacha mara moja tabia hiyo.

Gondwe amesema zipo taarifa za kuwepo tabia ya wanaume [mafataki] na wazazi wanaowakatisha masomo wasichana makusudi watu hao lazima waadhibiwe .

Mkuu huyu wa wilaya amesema kuwa wale wote ambao watakaobainika kurudisha nyuma juhudi za wanafunzi lazima waadhibiwe ili kutimiza lengo nakumkomboa mwanamke katika juhudi za ujenzi wa taifa na maendeleo kiujumla.

"Yoyote atakaye sababisha mwanafunzi asimalize masomo yake lazima tutamshughulikia ",alimalizia Gondwe.