Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:32 pm

WAANGALIZI WA UCHAGUZI WAIANDIKIA NEC BARUA KUHOJI SABABU ZA KUONDOLEWA

Habarileo

Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania yameiandikia barua Tume ya Uchaguzi nchini hapa kutaka maelezo yakwanini, yameondolewa katika orodha ya waangalizi wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Uchaguzi Zanzibar; Wapiga Kura Wagawanyika! | TanzaniaLeo

Hatua hii imekuja baada ya mashirika hayo pia kuondolewa katika mashirika zaidi ya 200 yanayotarajiwa kutoa elimu ya upigaji kura kwa wananchi.

Miongoni mwa mashirika hayo yaliondolewa katika orodha hiyo ni pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu pamoja na muungano wa mashirika ya kiraia nchini humo.

Hata hivyo vyama vya upinzani nchini Tanzania vinasema vitashiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba licha ya madai ya kunyanyaswa na vyombo vya Dola na kutokuwa na imani na Tume ya Uchaguzi.

Chama kikuu cha Upinzani nchini humo cha CHADEMA kimesema kitang'ang'ana kama ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita, huku Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia akionyesha wasi wasi wake kuhusu uchaguzi huo.

Kwa upande wake Chama kingine cha upinzani cha ACT Wazalendo kinasema wapo tayari kwa Uchaguzi huu licha ya tume iliyopo hivi sasa kutokuwa huru.

Kwa upande wake Chama kilichopo Madarakani CCM kinasema “kila kitu kipo sawa, zingine ni porojo”.

Imesalia miezi mitatu kufanyika uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na madiwani nchini Tanzania ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.