- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
UTAFITI: Je? Nikweli mwenza wako akisema amechoka kufanya mapenzi anakuwa amemanisha
England: MARA zote maneno ya kuashiria uchovu katika uwanja wa sita kwa sita kama “sitaki sasa, mpenzi, jamani mpenzi, nimechoka baby,” limekuwa likizungumziwa kwa muda mrefu na wapenzi ambao wanaonekana kuchoshwa na kile wanachoona kama kisingizio kwa upande wa wapenzi wao mradi tu wasifanye mapenzi.
Utafiti uliofanywa kwa wanawake zaidi ya 93,000 umegundua kwamba, usingizi mzuri huongeza sana hamu ya kufanya mapenzi na hivyo kuwafanya wafurahie tendo hilo.
Wale waliochoka, hata hivyo, walisema kuwa hawana furaha katika maisha yao ya kimapenzi.
Utafiti uliofanywa na taasisi ya North American Menopause Society NAMS) ilifanya uchambuzi wa takwimu zilizopatikana kwa wanawake wenye umri kuanzia miaka 50 hadi 79.
Watafiti wanasema kwamba matokeo yanaonyesha kuwa upo uhusiano wa moja kwa moja baina ya usingizi wa muda mfupi, dalili za kukosa usingizi au insomnia na kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi baada ya wanawake kupita umri wa kuzaa, yaani menopause.
Miongoni mwa wanawake walioshiriki katika utafiti huo, asilimia 56 walisema kuwa “wanaridhika kiasi” au “wanaridhika sana” na ufanyaji wa mapenzi, wakati kwa ujumla asilimia 52 walisema wamefanya mapenzi na wenza wao angalau mara moja katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Chini ya theluthi moja ya washiriki walisema wanakabiliwa na matatizo ya kupata usingizi, ambalo ni tatizo kubwa kwa wanawake waliovuka umri wa kuzaa, yaani walioingia kwenye menopause, tatizo ambalo linaweza kusababisha shinikizo la damu na msongo wa mawazo.
Utafiti huo pia uligundua kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya usingizi mzuri na wa kutosha na kuridhika kimapenzi hata baada ya kuhusisha mambo mengine ambayo yanasababisha ukosefu wa usingizi, kama msongo wa mawazo na magonjwa sugu.
Wakati ukosefu wa usingizi hupunguza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake, hata hivyo haikupunguza idadi ya siku ambazo walifanya mapenzi na wenza wao, utafiti huo uligundua.
Watafiti walisema kwamba tatizo sugu la ukosefu wa usingizi unamaanisha kwamba wanawake wanaweza kuendelea na shughuli zao za kila siku, ikiwemo kufanya mapenzi, lakini hali yao ya kufurahia na kuridhika nalo inapungua kutokana na kukosa usingizi.
Dkt. Joann Pinkerton, Mkurugenzi Mtendaji wa NAMS, alisema, “Kuna njia kadhaa za matibabu kusaidia ukosefu wa usingizi na kutoridhika kimapenzi, ikiwemo pamoja na matumizi ya homoni, njia ambayo utafiti huo umegundua kwamba inafaa sana kwa wanawake ambao wameshapita umri wa kuzaa.”
“Wanawake pamoja na watoa huduma za afya wanapaswa kutambua uhusiano baina ya dalili za menopause na ukosefu wa usingizi wa kutosha na jinsi zinaweza kuathiri furaha katika tendo la ndoa.”