November 23, 2024, 8:02 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
TAFITI: Buibu Kutumika kama Dawa ya KIHARUSI Duniani
Queensland: Wanasanyasi walifanya utafiti waligundua kwamba tiba ya protini katika sumu ya buibui inaweza kusaidia kulinda ubongo kutokana na jeraha baada ya kiharusi kulingana na protini hii ilifanya kazi ilipotumiwa katika panya wa maabara.
Wanasema kuwa ilionyesha kwamba inaweza kuwa tiba nzuri ya kiharusi katika siku za usoni lakini haijajaribiwa miongoni mwa binadamu.Muungano unaopigana dhidi ya ugonjwa wa kiharusi umesema kuwa utafiti huo bado ungali katika awamu ya kwanza lakini unaunga mkono tiba yoyote inayoweza kupunguza uharibifu unaofanywa na kiharusi.Watafiti kutoka chuo kikuu cha Queensland and Monash , walisafiri hadi kisiwa cha Fraser nchini Australia kuwawinda na kuwashika buibui hatari wa taifa hilo.Baadaye waliwachukua buibui hao katika maabara ili kuwatoa sumu hiyo.Hatua hiyo ilishirikisha kuwabembeleza buibui hao kutoa sumu hiyo ambayo baadaye hutolea kwa kupitia bomba Walitoa protini hiyo na kutengenezwa kadhaa katika maabara Baadaye walimdunga panya protini hiyo ambapo iliweza kuzuia jeraha lolote katika ubongo.