- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : PAMOJA NA UPUNGUFU WA WACHEZAJI YANGA KAZI MOJA USIKU WA LEO
Kikosi cha Yanga ambacho asilimia kubwa kinaungwa na vijana wasio na majina makubwa kwenye soka la Tanzania, kinatarajiwa kuanza kazi ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, leo kwa kukipiga dhidi ya U.S.M. Alger ugenini.
Mchezo huo unaotarajiwa kuanza majira ya saa nne usiku kwa hapa Afrika Mashariki ni wa Kundi D, utapigwa kwenye Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers.
Jana jioni kikosi cha Yanga kilifanya mazoezi ya mwisho uwanjani hapo licha ya hali ya hewa ya baridi.
Yanga inaongozwa na Kocha Mkongo, Mwinyi Zahera anayesaidiwa na Mzambia, Noel Mwandila na wazawa Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali ambaye ni kocha wa makipa.
Kikosi cha Yanga kinaundwa na vijana wengi kwa kuwa wale mastaa kina Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Ibrahim Ajib na Obrey Chifrwa hawakuongozana na timu kutokana na sababu mbalimbali.