- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : MKWASA AFUNGUKA BAADHI YA TIMU KUTOFUATA KANUNI KWENYE USAJILI
Wakati vuguvugu la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu Bara likiendelea hivi sasa, Katibu Mkuu klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa, amefunguka kwa kusema timu zinazosajili hivi sasa zinakiuka kanuni.
Kwa mujibu wa Radio One, Mkwasa ameeleza kuwa klabu zinazosajili zinaenda kinyume na taratibu kwasababu dirisha rasmi la usajili halijafunguliwa.
Katibu huyo amesema hayo kufuatia timu mbalimbali haswa za ligi kuu kuendelea na usajili wa wachezaji ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya awali.
"Unajua klabu zinazosajili hivi sasa zinaenda kinyume na utaratibu wa usajili, na hii yote ni kwasababu dirisha bado halijafunguliwa" alisema.
Mpaka sasa Yaanga haijaweka wazi ni wachezaji gani imewasajili zaidi ya kusikia tetesi zinazodai tayari imeshamalizana na mchezaji wake wa zamani, Mrisho Khalfan Ngassa.