- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWAN KIKWETE AWACHANA YANGA KUWA HAWEZI KUCHUKUA TIMU HIYO
Muda mfupi baada ya taarifa kusambaa kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete anatajwa kuwa anaweza kuwania nafasi ya uenyekiti wa Klabu ya Yanga, kiongozi huyo wa siasa amejitokeza na kuzungumza.
Ridhiwani Kikwete ambaye anajulikana na wengi kuwa ni mdau wa klabu hiyo amekuwa akitajwa mara kadhaa lakini safari hii jina lake limetajwa kwa ukubwa zaidi kuhusu kugombea nafasi hiyo ambayo imekuwa wazi kwa takribani mwaka mmoja sasa.
Ridhiwani ametoa kauli kwa kusema kuwa hana mpango huo wa kugombea na wala hajawahi kufikiria kuwania nafasi hiyo ya juu klabuni hapo.
Yanga ambayo makao makuu yake yapo Jangwani mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, kwa muda imekuwa chini ya Kaimu mwenyekiti, Clement Sanga ambaye anashika nafasi hiyo iliyoachwa wazi naYusuf Manji aliyejiuzulu kutokana na sababu binafsi.
Manji aliachia ngazi, mwezi wa tano mwaka 2017 kwa kile alichodai anaacha nafasi kwa wengine baada ya kuiongoza Yanga kwa muda. Awali ilionekana anatikisa kibiriti, lakini muda ulivyosonga ndipo watu wakajua yupo ‘serious’.
Akizungumzia hilo la uenyekiti, Ridhiwani amesema kuwa kwanza ili ugombee nafasi hiyo lazima uwe mwanachama wa Klabu ya Yanga na hivyo yeye hana vigezo.
“Kwa sasa nina majukumu mengi na ikumbukwe kuwa mimi siyo mwanachama wa Yanga ni shabiki tu mkubwa wa Yanga, niliwahi kutoa maoni yangu juu ya uendeshwaji wa timu wakati ule wa Manji, lakini kuna walionipinga na kuniona nazungumza vitu ambavyo haVifai na sina mamlaka hayo kwa kuwa wao walikuwa wakipata sukari.
“Hivyo, niseme tu kuwa sina mpango huo kwa sasa na wala sifikirii licha ya kuwa mimi ni mdau mkubwa wa Yanga,” alisema Ridhiwani.