- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : BANDA APANIA MSIMU UJAO WA LIGI KUU AFRIKA KUSINI
BEKI wa Baroka FC, mtanzania Abdi Banda amepania kufanya vizuri msimu mpya wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini baada ya kudai kuwa tayari ameifahamu vizuri ligi hiyo.
Banda alijiunga na timu hiyo akitokea Simba,na kuwa mchezaji wa tatu kucheza nje ya nchi,baada ya Samatta na Msuva.
Banda ni miongoni mwa wachezaji ambao katika kikosi cha Baroka hawakuanza kucheza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani na ugeni katika timu hiyo.
Akizungumza na Gazeti hili Beki huyo tegemezi wa Taifa Stars alisema kuwa kutokana na kuifahamu Ligi hiyo ndani ya muda mufupi ana imani ya kufanya vizuri msimu ujao.
Ndani ya Kipindi kifupi alichojiunga na timu hiyo alisema kuwa Mwalimu Kgoloko Thobejane ameonesha kumuamini,hivyo ni muda wake wa kuonesha uwezo wake.
"Kikubwa nishaijua Ligi ya South Africa na nadhani huu ndio muda wa mimi kuonesha uwezo wangu nilionao maana sasa nimeaminiwa,"alisema Banda.
Alisema nafasi hiyo imekuja kama bahati maana,kabla ya hapo hakuaminiwa kama ilivyo sasa,hali iliyomfanya ashindwe kuonesha uwezo wake.
Tangu kusajiliwa na timu hiyo,nyota huyo wa zamani wa Simba amefunga magoli matatu,akifanya hivyo dhidi ya Orando Pirates na Bloemfontein Cetic baada ya kufunga
mawili.