- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: SERGIO RAMOS: MOHAMED SALAH ALIJITAKIA MWENYEWE KUUMIA
Hispanaia: Baki wa wa kimataifa wa timu ya taifa ya Hispania na club ya Real Madrid Sergio Ramos amesema kitendo cha mshambuliaji wa Liverpool Mohamed salah kuumia kwenye bega kilikuwa cha kujitakia mwenyewe baada ya mchezaji huyo Rai wa Misri kuanza kumshika mkono katika fainali ya ligi ya mabigwa Barani Ulaya.
Ramos, 32, amezungumza jana June 6 wakti akihojiwa na AS: "huu ni Upuuzi mtupu, watu wengi waliangalia upande mmoja tu wa Salah sana. Sikutaka kuzungumza kwa sababu kila kitu kimeongezwa chumvi kwenye tukio lile."
Kila nikiutazama mchezo ule vizuri, naona Salah anaushika mkono wangu kwanza na ninaanguka upande mmoja, na jeraha lilitokea kwenye mkono ule mwingine na wanasema kwamba nilishika mkono na kuuvunja kama mchezaji wa judo. na Baada ya hapo, kipa wao tena alisema nilimduwaza kwa kumgonga" aliongea Ramos
"Kitu pekee sijasikia ni Roberto Firmino akisema kwamba alipata mafua kwa sababu aliangukiwa na jasho langu," amesema Ramos kwa kutania.
Ramos pia amedai kwamba Salah angeendelea kucheza mechi hiyo "iwapo angedungwa sindano kipindi cha pili".
"Niliwasiliana na Salah kupitia ujumbe, alikuwa vyema. Angeendelea kucheza iwapo angedungwa sindano kipindi cha pili. Nimefanya hivyo mara kadha lakini wakati ni Ramos alifanyajambo kama hilo, linakwamilia zaidi.
Salah, 25, aliondoka uwanjani akitokwa na machozi baada ya kuumia begani kwenye fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya huku Real Madrid waliwalaza Liverpool 3-1 kwenye mechi hiyo iliyochezewa Kiev, Ukraine.
Mchezaji huyo baadaye alifanyiwa upasuaji.
Ramos pia aligongana na kipa wa Liverpool Loris Karius ambaye inadaiwa alipata jeraha kwenye ubongo kabla yake kufanya makosa mawili yaliyochangia Real kufunga.
Imeandikwa na Issa Deyssa na kuhaririwa na Zawadi Machibya (muakilishi Publisher)