Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 10:48 pm

SPORT: PENDEKEZO LA KUWEPO TIMU 48 KWENYE KOMBE LA DUNIA LAPITISHWA

Shirikisho la soka Duniani FIFA limefanya mabadiliko ya Kimuundo katika shirikisho hilo, mabadiliko hayo yamekuja baada ya Rais wa shirikisho hilo Bw.Gianni Infantinokutoa mapendekezo ya kuongeza idadi ya timu washiriki katika michuano ya kombe la Dunia, kwa maana hiyo timu 48 zitashiriki kwenye kinyang'anyiro cha kombe la Dunia. Infantino alikuwa na Ndoto ya kuwepo na washiriki wengi zaidi kwenye kombe la dunia ili kuzipa motisha timu zingine kushiriki na hii ilikuwa ni Ahadi yake wakati anaomba kura kabla ya uchaguzi.


Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.

Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.

Mwezi januari chama hicho chenye mamlaka makubwa ya soka duniani, kilipanga kuongeza timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia kutoka 32 mpaka 48 na hii itaanza mwaka 2026

MCHANGANUO UPO HIVI

Afrika - 9 kutoka timu za awali 5

Asia - 8 kutoka timu 4 za awali

Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali

Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali

Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali

Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali