- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: KOCHA REAL MADRID ZIDANE AJIUZULU
Uhispania: Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amejiuzulu nafasi yake kama mkufunzi mkuu katika club hiyo ya nchini Uhispania ambapo ni siku tano tu baada ya kuiongoza Real kushinda Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Zidane aliambia mkutano na vyombo vya habari kwamba kila kitu kinabadilika na kwamba hiyo ndio sababu ya uamuzi wake
Anaondoka baada ya kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji matatu ya klabu bingwa na taji moja la ligi ya La Liga tangu achukue hatamu mnamo mwezi Januari 2016.
''Naipenda klabu hii'', aliongezea.
''Kile ninachofikiria ni kwamba timu hii inafaa kuendelea kushinda ,lakini nadhani inahitaji mabadiliko , sauti mpya, mbinu mpya. Na hiyo ndio sababu ilionisukuma kufanya uamuzi huu''.
Zidane, 45, alichukua uongozi wa klabu hiyo baada ya Rafael Benitez kufutwa kazi na alisimamia mechi 149 games.
Aliisaidia Real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia 69.8% ya ushindi mbali na mataji tisa.
Alisema mnamo mwezi Januari kwamba ataondoka katika klabu hiyo atakapohisi kwamba hana la ziada kuisaidia timu hiyo.
Hatahivyo , tangazo linaonekana kuwashangaza wengi kwa kuwa linajiri siku chache tu baada ya Real kuishinda Liverpool 3-1 katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya
"Hii ni klabu ambayo imeshinda mataji 13 ya Ulaya , kwa hivyo nafurahia kuwa miongoni mwa historia yake'', alisema baada ya ushindi mjini kiev.
Tutafikiria kuhusu kile tulichofanikiwa kufanya. Tufurahie. Huu ndio wakati muhimu zaidi.
"We are going to think about what we achieved, enjoy the moment first. This is the most important thing now."