- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: Messi afungiwa mechi nne kwa kumtusi mwamuzi
Argentina: Mshambuliaji wa Club ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi amefungiwa kucheza mechi nne za kimataifa,kwa kosa la kumtukana mwamuzi msaidizi wakati wa mechi kati ya Argentina na Chile siku ya Alhamisi mjini Buenos Aires.
Shirikisho la soka duniani FIFA, lilitangaza uamuzi huo saa chache kabla ya Argentina kukutana na Bolivia katika mechi muhimu ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao. Argentina, walionekana kumkosa sana mshambuliaji huyo wa Barcelona, na walilazwa 2-0 katika mechi hiyo iliyochezewa mji wa La Paz.
Mabao ya Bolivia yalifungwa na Juan Carlos Arce na Marcelo Martins.
Kwa sasa, Argentina wanashikilia nafasi ya nne.
Zikiwa zimesalia mechi nne za kufuzu,
Argentina wanakabiliwa na hatari ya kushindwa kufuzu kwa michuano hiyo itakayoandaliwa nchini Urusi.
Timu nne za kwanza Amerika Kusini ndizo huhakikishiwa nafasi ya kucheza michuano hiyo.
Colombia walipanda juu ya Argentina na Uruguay na kutua nafasi ya pili kwa kulaza Ecuador 2-0 kupitia mabao ya James Rodriguez na Juan Cuadrado.
Argentina huenda wakatolewa nafasi ya nne iwapo Chile watafanikiwa kuwalaza Venezuela baadaye.
Uruguay watakuwa pia uwanjani dhidi ya Peru nao Brazil wanaoongoza wakutane na Paraguay.