Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:27 pm

SPORT: MABAO YA KUJIFUNGA YAMECHUKUA UMAARUFU KOMBE LA DUNIA URUSI

Goli la Own goal' limepata umaarufu mkubwa sana katika mechi za Iran, Ufaransa, Croatia, Senegal na Russia.

Ingawa kombe la dunia la Ufaransa 1998, lilishuhudia mabao sita ya kujifunga , sasa kwenye shindano nzima, la nchini Urusi, baada ya mechi 17, mabao ni matano tayari.

Baada ya mechi zote, magoli ya kujifunga yalikuwa 6 mwaka wa 1998. Tumesalia na zaidi ya mechi 40 na mabao ni 5.

Mabao ya 'Own goal yalikuwa hivi'

Iran (v Morocco), 15 Juni 2018

Own Goal alipata bao lake la kwanza kwenye mechi kati ya Iran na Morocco,tarehe 15 Juni.

Kiungo wa Morocco Aziz Bouhaddouz alijifunga baada ya kuingia na kuipa Iran ushindi mechi ya kwanza kundi B.

Ufaransa (v Australia), 16 Juni 2018

Own goal alipaa bao lake la pili kipute cha kundi C.

Beki wa Australia Aziz Behich naye alijifunga wakaicheza dhidi ya Ufaransa siku iliyofuata tarehe 16 Juni

Ilikuwa mechi ya ufunguzi kundi C

Goli hilo lilikuwa na umuhimu kwani liliipa Ufaransa ushindi na alama 3.

Croatia (v Nigeria), 16 Juni 2018

Goli la tatu la mchezaji Own Goal Urusi 2018.

Kiungo wa Nigeria Oghenekaro Etebo alikuwa wa tatu kujifunga wakichuana na Croatia.

Croatia's first goal in their 2-0 win in Group D.

Alielekeza kona ya Luka Modric langoni na kuwa goli la kwanza la Croatia.

Senegal (v Poland), 19 Juni

Senegal ilipata uongozi dhidi ya Poland kufuatia goli la wenyewe lililofungwa na Thiago Cionek.

Kiungo mkabaji wa Senegal Idrissa Gueye aliachilia kombora lililoelekezwa langoni na beki Cionek mechi ya Kundi H.

Russia (v Misri), 19 Juni

Own Goal alikuwa wa kwanza kufunga safari hii kwneye mechi hiyo ya kundi A. Aliisaidia Russia kukaribia kufuzu kwa hatua ya muondoano.