- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: CHELSEA KUITAZAMA UEFA KWA JIRANI
England: Club ya Chelsea hatimaye imekubali kutocheza ligi ya Mapingwa barani ulaya (UEFA) baada ya jana kuchezia kichapo cha kushangaza kutoka kwa Newcastle United cha mabao 3 -0 nakuifanya club hiyo kumaliza ligi kwa pointi 70 , pointi 5 nyuma ya majogoo wa jiji Liverpool.
Jana Chelsea walitakiwa kuomba dua mbili kwa wakati mmoja, huku wakiomba waifunge Newcastle wakati huo huo wakiombea Liverpool Kupoteza game yao, Dua ambayo ilienda vise-verse(kinyume) wakapokea kichapo wao na Liverpool ikashinda kwa maana hiyo sasa Chelsea watacheza Europa League baada ya kumaliza nafasi ya tano na kubaki kama mashabiki kwenye Ligi ya mabingwa barani ulaya (UEFA).
Vijana wa Antonio Conte hao sasa macho yao kwa kiwango kikubwa yanaelekezwa kwenye fainali ya Kombe la FA Jumamosi dhidi ya Manchester United.
Ushindi wa Liverpool hata hivyo haukutosha kuwafikisha nafasi ya tatu kwenye jedwali ambayo ilitwaliwa na Tottenham waliopata ushindi wa 5-4 dhidi ya Leicester kwenye mechi ambayo huenda ikawa yao ya mwisho kuchezea Wembley kama uwanja wao wa nyumbani kabla ya kuhamia uwanja wao mpya White Hart Lane.
Vijana hao wa Mauricio Pochettino walijipata nyuma mara tatu, lakini Erik Lamela na Harry Kane walifunga mabao mawili kila mmoja, Kane akifikisha magoli 30 ligini, naye Christian Fuchs akajifunga na kuwapa ushindi.