- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: CHAMA CHA SOKA CHA GHANA CHAVUNJWA KWA VISA VYA RUSHWA
ACCRA: Serekali ya Ghana imekivunja chama cha soka cha nchi hiyo baada ya rais wa chama hicho Bw. Kwesi Nyantakyi kunaswa katika video akionekana kupokea 'zawadi ya pesa' ya $65,000 kutoka kwa mwanshi wa habiri mmoja aliyejifanya kama mfanyibiashara aliye na shauku ya kuwekeza katika soka la nchini humo.
Mpaka sasa Bw. Kwesi Nyantakyi hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo za rushwa.
Mtandao wa wa Ghanaweb Umeripoti kuwa Waziri wa michezo wa nchi hiyo Isaac Asiama amesema chama hicho 'kimevunjiliwa mbali mara moja'.
Waandishi wanasema uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi habari anayekumbwa na mzozo Anas Aremayaw Anas umezusha maswali kuhusu soka barani Afrika.
Katika makala hiyo ndefu, iliopewa jina 'wakati ulafi na rushwa zinapokuwa kawaida', ilikabidhiwa kwa maafisa wa serikali mwezi uliopita na kuonyeshwa wazi mbele ya umma kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.Kwesi Nyantakyi
Mustapha Abdul-Hamid, waziri wa habari Ghana amesema serikali "imeamua kuchukua hatua za mara moja kukivunja chama cha soka Ghana GFA", akitaja "kuenea kwa muozo unoaonekana".
Amesema hatua za muda za kuongoza soka Ghana zitatangazwa hivi karibuni, kukisubiriwa kuundwa chama kipya.
Katika taarifa yake GFA kimesema itatoa ushirikiano katika uchunguzi wowote.
Mustapha Abdul-Hamid
Nyantakyi ni makamu wa rais wa shirikisho la kandanda Afrika na pia mwanachama katika baraza la Fifa - taasisi inayosimamia soka duniani.
Tangu achukuwe uongozi wa chama cha GFA, ametuma ujumbe mkuu dhidi ya kupambana na rushwa.
Hatahivyo katika makala hiyo ya upekuzi inamuonyesha akiweka pesa hizo $65,000 "za kununua vitu" katika mfuko mweusi wa plastiki.