Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:50 pm

RIPOTI: Tanzania yawekwa Miongoni mwa nchi zisizo na furaha Duniani

Norway: Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani. Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani wake Denmark, ambayo imechukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita.

Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya kati ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani.

Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19.

Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini. Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147 mtawalia