Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 2:55 am

RAIS MUSEVENI: ITAKUWA NI WENDAWAZIMU KUFANYA UCHAGUZI NA CORONA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa itakua ni 'uendawazimu' kuendesha uchaguzi wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akiliambia shirika la habari la Uganda NBS kwamba mipango ya kufanya uchaguzi mapema mwaka 2021 haitakuepo kama virusi vya corona havitadhibitiwa itatakiwa kuangaliwa upya.

COVID-19: Museveni extends lockdown for more 14 days – Watchdog Uganda

Nchini Uganda Kuna jumla ya visa 129 vya Covid-19 vilivyothibitishwa nchini humo.

Mikutano ya umma mkiwemo ya kisiasa imepigwa marufuku kama sehemu ya hatua za kutosogeleana na kukaa nyumbani zilizowekwa nchini humo kwa ajili ya kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.

Takriban wagombea 24 wametangaza nia yao ya kugombea kiti cha urais na wamewasilisha maombi yao kwa Tume ya Uchaguzi ili kukabiliana na rais Museveni na wameanza mikutano ya kitaifa.

Mikutano hii imeahirishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Kauli za Bwana Museveni sasa zimeibua swali juu ya ikiwa mchakato mzima wa uchaguzi utaahirishwa au la.

Kumekua na maswali juu ya ni kwa kiwango gani uchaguzi huo utakua ni wa haki na huru huku kukiwa na shutuma kwamba wapinzani wa Museveni walikabiliwa na vitisho.

Jenerali mstaafu , Henry Tumukunde, ambaye alitangaza mipango ya kukabiliana na Museveni ambaye alikua mshirika wake zamani pia ameshitakiwa kwa mashtaka ya uhaini na kuachiliwa kwa dhamana siku ya Jumatatu baada ya kukaa jela miezi miwili.