Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:45 pm

Rais Kenyetta ataka wabunge wote kupunguziwa mishahara

Nairobi: Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa wito wa kupunguzwa mishahara ya wabunge na maafisa wakuu akisema suala hilo limechangia kuzuka kwa migomo ya wafanyakazi wengi wa uma kutaka mishahara yao iongezwa angalau wawafikie wabunge kwani inaonesha wabunge wengi wa Africa wanapokea mishahara mikubwa sana kiasi Cha kuwa na tofauti kubwa kati ya mfanyakazi wakawaida wa serekali na wabunge.

Rais Kenyatta ameyasema hayo alipohutubia kwenye kikao cha pamoja cha Bunge la Taifa na Baraza la Senate katika hotuba yake ya mwisho ya kipindi chake cha kwanza uongozini na kuongeza kuwa viwango vya juu vya mishahara ya wabunge vimesababisha migomo ya wafanyakazi wa sekta nyingine kutaka nyongeza za mishahara.

Hotuba ya Rais huyo imesheheni majibu ya maswali yanayoulizwa na upinzani kila uchao kuanzia ufisadi, ufujaji wa fedha za umma, kuzorota kwa huduma za afya, elimu na usalama.

Rais Uhuru amejivunia kupungua kwa visa vya mashambulizi ya magaidi nchini, kuongezwa kwa idadi ya maafisa wa usalama na ukuaji wa uchumi ambao amesema umekuwa juu ya kiwango cha makadirio ya taasisi za kimataifa cha asilimia tatu kwa Mwaka.Rais Uhuru ametaja mmoja baada ya mwingine miradi ambayo serikali yake imetimiza katika kipindi cha miaka minne uongozini. Lakini pamoja na yote kauli iliyoibua hisia ni ile ya kutaka mishahara ya wabunge na maafisa wakuu wa serikali ipunguzwa.

Amesema viwango vya juu vya mishahara ya wabunbe vimewafanya wafanyakazi katika sekta nyingine kupigania nyongeza za mishahara. Huku zikiwa zimesalia siku 145 uchaguzi mkuu kufanyika Rais Uhuru Kenyatta amechukua fursa ya hotuba hiyo kujipigia upatu ili aweze kuchaguliwa tena kwa kipindi cha pili.

Kinyume na hotuba ya Mwaka uliopita, hotua ya Mwaka huu haikutatizwa na wabunge wa upinzani kama walivyokuwa wameapa kufanya ikiwa Rais hangeomba msamaha wananchi kwa matamshi yake ya matusi katika siku za hivi karibuni. Hata hivyo hilo lilipingwa na mbunge wa Mvita.