- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
PROF LIPUMBA: TUNDU LISSU ANATAFUTA KIKI YA KISIASA.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kisipewe madaraka kwani hakina sifa ya kuongoza nchi.
Prof Lipumba ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama hicho amesema CHADEMA inapaswa kijitafakari kwa Mgombea waliyemsimamisha inawezekana baada ya kupata ajali amepata matatizo ya akili kwani hoja alizozitoa Tume ya Uchaguzi dhidi yake hazina mashiko.
“Sisi tunasimama kusimamia Demokrasia lakini cha ajabu CHADEMA inaniwekea pingamizi, hii ni dhahiri hoja zangu hawaziwezi kwanini waniwekee pingamizi mimi. Kama CHADEMA wapo vizuri basi washindane kwa hoja na sio kuweka pingamizi zisizo na maana kwani hii haijengi demokrasia ya kweli”
Pia Prof Lipumba, amesema Tundu Lissu amekufa kisiasa hivyo anatafuta sababu ya kiki ili aanze upya katika ulimwengu wa siasa, anaona njia inayofaa ni kuleta taharuki kwa wanachama wa CUF.
Lipumba ametoa kauli hiyo baada ya kuona taarifa kuhusu Tundu Lissu kumuwekea pingamizi kwa Tume ya Uchaguzi (NEC) la kumtaka asigombee ingawa Tume ya Taifa ya Uchaguzi lilitupilia mbali pingamizi lake kwakuwa halikuwa la kisheria na Lipumba hakuwa na kosa kwenye ujazaji wa fumu ya Urais.