- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:TWAWEZA WAPEWA SIKU 7 ZA KUJIELEZA KUTOA TAARIFA BILA KIBALI
Dar es Salaam: Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imeitaka Taasisi ya Twaweza kujieleza ndani ya siku saba kwa nini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kosa la kutoa matokeo ya utafiti bila ruhusa.
Barua hiyo ya Costech imesema, Twaweza waliomba kibali cha tafiti nne ambazo mmoja umekamilika na nyingine tatu bado zinaendelea.
Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosambaa mitandaoni ikionyesha imesainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu, tume hiyo ndiyo yenye mamlaka ya kusajili na kutoa kibali cha tafiti zote za muda mfupi na mrefu zinazofanywa nchini.
Barua hiyo imedai kuwa mwishoni mwa wiki, kulikuwa na taarifa za Twaweza kutoa utafiti uliopewa jina la ‘Sauti za Wananchi’ ambao, tume haina rekodi zilizoruhusu kuchapishwa kinyume cha sheria.