Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 11:53 pm

NEWS: ZITTO AHUKUMIWA KUTOSEMA MANENO YA KICHOCHEZI KWA MWAKA 1

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemkuta na hatia Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe katika makosa yote matatu ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili, Mahakama hiyo imemuachilia huru kwa sharti moja kubwa la kutotoa ama kuandika maneno yaeyote ya kichochezi kwa kipindi cha mwaka moja.

Leo asubuhi Mbunge huyo wa Kigoma Mjini aliwasili Mahakamani hapo pamoja na Mawakili wake, (Jebra Kambole na Grece Mapunda ) kusubiri hukumu dhidi ya kesi yake hiyo na akiwa tayari amesha nyoa kipara ikimaaninsha yupo tayari kwenda Jela kutumikia kifungu ikiwa Mahakama itamuamuru kifungu cha kwenda Jela.

Hukumu hiyo ya kesi ya uchochezi, iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Haruna Shaidi iliyotolewa leo mei 29, 2020 imevuta hisia za watu wengi ndani na nje ya Tanzania.

Kesi hiyo ya Zitto iliyofunguliwa mnamo tarehe 2 Novemba 2018 na Jamhuri ya Tanzania, akituhumiwa kutoa maneno ya Uchochezi.

Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo, alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Mashtaka ya Zitto yanatokana na kauli zake za kulitaka jeshi la polisi kutolea maelezo kile alichokiita mauaji ya polisi na raia yaliyotokea kwenye Kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma.