November 30, 2024, 7:44 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZIFAHAMU SABABU MAALUM ZA BURUNDI KUFUNGIA BBC NA VOA
Bujumbura: Jana Serikali ya Burundi imeonya na kuchukua hatua ya kupiga marufuku matangazo ya mashirika ya utangazaji ya BBC na VOA kwa muda wa miezi sita kuanzia Mei 7 mwaka huu.
Mashirika haya ya utangazaji yanashtumiwa na serikali ya Burundi kutofuata sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari hapo nchini.
Serikali ya Burundi inaishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo.
Mtandao wa habari unaoegemea upande wa serikali ya Burundi, Ikiriho, kwenye ukurasa wake wa Twitter, umerusha nyaraka ya taarifa hiyo.
Radio kadhaa za kibinfasi zimeharibiwa na kufungwa nchni humo wakati wa mzozo wa kisiasa ulioanza mnamo 2015, wakati rais Nkurunziza aliposhinda muhula wa tatu madrakani, uliozusha mgogoro wa kisiasa na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kuyahama makazi yao. Watu zaidi ya 3000 wamezuiliwa katika jela mbalimbali kwa mujibu wa mashirika ya kiraia nchini humo
Nchi hiyo inajitayarisha kwa kura ya maoni Mei 17 ambayo huenda ikamuongezea muda wa kuhudumu rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch linasema vikosi vya serikali ya Burundi na wafuasi wa chama tawala wamewaua , kuwapiga na kuwatesa watu wanaowaona kama wapinzani wa kura hiyo ya maoni.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani hivi karibuni imesema huenda kura hiyo ikaathiri taasisi za demokrasia nchini humo
Newest Posts