- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Zaidi ya Carton 3,000 za Viroba zakamatwa Mkoani Dodoma
Dodoma : Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa kushirikiana na mamlaka zingine za Serekali zimefanikiwa kukamata shehena za viroba catoni 3,972 zenye thamani ya shilingi milioni 354,457,000.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Godaoni la kampuni ya TAKAWEDO Investment maeneo ya Kisasa manispaa ya Dodoma Mjini kamanda wa polisi mkoa wlilia Dodoma Lazaro Mambosasa Amesema "kwa kushirikiana na vyombo vya Dola, mamlaka ya chakula na dawa TFDA Imefanikiwa kuwakamata ALEXNDER S/O LIPINDO Miaka 52 Na WILLIAMS/O EDMUNDI LUPINDO Miaka 39 wakazi wa Dodoma mjini ambao ni wafanya Biashara mkoani hapa ambao wanajishuhulisha na Biashara ya Vinywaji mbalimbali.
Mambosasa ametaja aina ya pombe zilizokamatwa kuwa ni vifungashio vya plastics ambavyo ni konyagi caton 1,399, Valuer caton 712, Kiroba Orrginal caton 1,782, Bismark caton 24, zanzi Caton 55. jumla ya caton zoteni 3,972.
Ameongeza kwa kusema kuwa shehena hiyo imezuiliwa kwa kuwekewa utepe maalumu ili isiweze kuondolewa na kusambazwa .